Back to top

“Pelekeni vifurushi vyenu vya huduma Bodi ya Utalii”Mhe.Kigwangala

21 November 2019
Share

Wadau wanaofanya biashara katika sekta ya utalii nchini wametakiwa kupeleka bodi ya utalii taarifa za vifurushi vyao vya huduma wanazotoa ili viweze kuwa sehemu ya matangazo kwenye viwanja zaidi ya 40 vinavyohudumiwa na kampuni ya huduma za viwanja vya ndege (NAS).

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe.Hamisi Kigwangalla wakati akishuhudia makubaliano ya utiaji saini wa ushirikiano wa kutangaza utalii wa Tanzania na kampuni ya NAS inayotoa huduma za viwanja vya ndege kwa ndege na abiria katika viwanja mbalimbali ulimwenguni.

Utekelezaji wa wito huo kwa wadau wa sekta ya utalii utasaidia kuonekana kwa taarifa zao kenye viwanja vya kimataifa vilivyo mashariki ya kati Asia na Afrika.