Back to top

Afariki baada ya kuanguka kwenye maji yaliyozingira nyumba.

21 November 2019
Share

Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam  zimesababisha kifo cha mtu mmoja katika  eneo la Stakishari Banana baada ya kuanguka ndani ya maji yaliyokuwa yamezingira nyumba za wakazi wa eneo hilo.

Mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Augustino Mwenga amepoteza maisha baada ya kuanguka wakati akiwa katika harakati za kujilinda na athari za maji kujaa katika eneo hilo.