Back to top

Arumeru wabuni Teknolojia ya kutumia nyuki kulinda vyanzo vya  maji.

09 June 2019
Share

Wilaya ya Arumeru imeanza kutumia teknolojia mpya ya kutumia nyuki kulinda vyanzo maji,teknolojia ambayo licha ya kulenga  kupunguza shughuli za binadamu kikiwemo kilimo katika vyanzo  hivyo pia itaongeza kipato kwa wananchi.

Akitoa ufafanuzi wa malalamiko ya wananchi ya kuendelea kuwepo  kwa uharibifu wa vyanzo vya maji ukiwemo wa kilimo na kuchunga mifugo mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw Jerry Muro amesema   wamebaini kuwa pamoja na hatua zingine zinazochukuliwa kwa  wahusika nyuki wakitumika vizuri wanaweza kusaidia kulinda  mazingira kwa kiasi kikubwa na pia kuwasaidia wananchi  kiuchumi.


Baadhi ya wananchi wamesema uharibifu wa mazingira katika  vyanzo vya maji bado ni mkubwa hasa wa kuingiza mifugo tatizo  ambalo athari zake zinaonekana wazi na kwamba jitihada za ziada zinahitajika.


Akizungumzia changamoto hiyo Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw Mkongea Ali ambaye ametembelea,kukagua na kuzindua miradi  mbalimbali ikiwemo ya uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji  amewataka viongozi na watendaji wa wilaya hiyo kutowaonea  huruma wanaochezea vyanzo vya maji kwani ni sawa na kuchezea  maisha ya watu.