Back to top

Ugonjwa ulivyokatisha ndoto zake,aomba msada akatibiwe nje.

22 August 2019
Share

Mkazi wa Kilwa Masoko, mkoani Lindi,bwa.Daud Lusian Kyangu miaka 32, ameiomba serikali pamoja na wadau wengine kumsaidia kiasi cha fedha ambacho kitamsaidia kusafiri  kwenda nje ya nchi kupata matibabu zaidi baada ya hospitali za ndani kutopata unafuu wa ugonjwa wa ngozi unaomsumbua kwa kipindi cha miaka 9 sasa.

Daudi amesema ugonjwa huo ulianza mwaka 2011 akiwa  anasomea Upadre Seminali ya Namupa, mkoani Lindi,na baada ya kupata ugonjwa huo ndoto zake ziliishia hapo nakuanza kuangaika hospitali mbalimbali za mkoa wa Lindi pamoja na mkoa wa Mtwara.

Amesema mwaka jana alienda hospitali ya Taifa ya Muhimbili walifanikiwa kumfanyia vipimo na walichukua nyama ya kisogoni pamoja na mgongoni kwa ajili ya uchunguzi na baada ya siku 21 ambazo alilazwa hospitalini hapo alipewa majibu kuwa  mwili wake una saratani ya ngozi yaani wadudu wako kwenye damu ikabidi apewe dawa nakurudi nyumbani.

Lakini toka apewe dawa hizo toka mwezi wa tisa mwaka jana  ametumia dawa ndani ya kipindi cha miezi sita,lakini hadi sasa hazijamsaidia chochote hali inaendelea kuwa mbaya mwilini mzima una mabaka mabaka tu.

Kifupi anachoomba Daud kwa Watanzania mbalimbali ikiwemo  Serikali,Makampuni na jamii kwa ujumla anaomba msaada wa kifedha ambao utamsaidia kusafiri kwenda nje ya nchi  kubitiwa inawezekana atapona huo ugonjwa unaomsumbua.

Anaetaka kumsaidia Daud Lusian Kyangu namba zake za simu ni 0687-714-244 kutoa ni moyo na si utajili leo kwake kesho kwa mwingine Mungu amsaidie aweze kupona ili aendelee na shughuli zake za kulijenga Taifa.