
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeiongezea bajeti Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA), Wilaya ya Busega iliyopo mkoani Simiyu kutoka shilingi milioni 500 hadi shilingi bilioni 2.4.
“Miaka minne iliyopita wilaya ya Busega ilikuwa na bajeti ya shilingi milioni 500 kwa mwaka, baada ya kuingia madarakani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan bajeti ya TARURA Wilaya ya Busega imepanda kutoka milioni 500 hadi bilioni 2.4 kwa nyongeza ya tozo bilioni 1.2, mfuko wa jimbo milioni 500, na mfuko wa barabara milioni 748 na kufanya jumla ya bilioni 2.4,”. Hayo yameelezwa na Meneja wa TARURA Wilaya ya Busega, Mhandisi Mathias Mgolozi.
Amesema, kutokana na nyongeza hiyo, TARURA imekuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi nyingi, ambapo kwa mwaka 2023/24 wametengeneza kilomita 100 kati ya kilomita 511 walizonazo kwenye mtandao wa barabara wilayani humo
