Back to top

Bilioni 50 zimetolewa kwa ajili ya mapambano ya ukimwi na kifua kikuu.

25 May 2018
Share

Serikali imejipanga kuhakikisha ifikapo mwaka 2022 asilimia 95 ya watu wote wanaoishi na virusi vya ukimwi pamoja na asilimia 90 ya watoto waliofikia vigezo na wanaoishi na maambukizi wanatumia dawa  za kufubaza maambukizi ya virusi vya ukimwi nchni nzima.

Akizungumza na ITV baada ya kushuhudia kusainiwa kwa Rasimu ya mikataba wa zaidi ya shilingi Bilioni 50 fedha za Mfuko wa Dunia kati ta AMREF na Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na sekta ya afya na vijana  kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukimwi na kifua kikuu,nNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,jinsi wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile ameyataka Mashirika hayo kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na kuzingatia kuwa inalenga kuwanufaisha mamilioni ya Watanzania.

Kwa upande Mkurugenzi mkazi wa  Shirika la AMREF Daktari Florence Temu amesema shirika hilo limekabidhiwa dhamana ya kusimamia fedha hizo za Mfuko wa Dunia kwa ajili ya kuibua na kutibu virusi vya ukimwi na kifua kikuu kupitia asasi za kijamii ambapo zaidio ya dola Milioni 24.9 zitatumika ili kuhakikisha kiwango cha asilimia 90 kinafikiwa katika kutokokeza kifua kikuu,kudhhibiti maambukizi pamoja na kuleta huduma katika ngazi ya jamii.