Ukaguzi wa magari mkoani Ruvuma uliofanywa na mamlaka ya usimamizi wa bima nyanda za juu kusini kwa kushirikiana na jeshi la polisi umebaini baadhi ya magari kutumia stika za polisi za kughushi huku magari mengine ya abiria yakitumia bima za magari ya kutembelea nyumbani.
Ukaguzi huo umefanyika katika kituo cha mabasi cha Songea mkoani Ruvuma na kubaini kasoro hizo hatua ambayo haikubaliki kisheria na pia inaleta usumbufu kwa abiria pindi inapotokea ajali.
Kamanda wa kikosi cha usalama bara barani mkoa wa Ruvuma mrakibu msaidizi wa polisi Salumu Morimori amesema suala la magari kuwa na bima ni takwa la kisheria na wanaokiuka takwa hilo pamoja na kuwa na stika za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wao madereva na abiria wamesema kuwa zoezi la ukaguzi wa bima na stika za polisi kwenye magari ni muhimu sana kwa kuwa linawasaidia abiria kulipwa fidia zao pindi itokeapo ajali na madereva inawasaidia kutii matakwa ya kisheria.