Back to top

DHAMIRA YA TANZANIA NI KUKUZA AMANI BARANI AFRIKA

25 May 2024
Share

 Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, amesema dhamira ya Tanzania ni kuendelea kukuza amani na usalama barani Afrika ili kuweka mazingira stahiki ya kujenga ustawi wa kijamii na kiuchumi kwa wananchi.

Rais Samia ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika ambalo linaadhimisha mia ka 20 chini ya uenyeji wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo kwa mwezi Mei mwaka 2024.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Rais Samia amesema tangu kuanzishwa kwa baraza hilo, amani na usalama umekuwa na nafasi muhimu katika kukuza  amani usalama na utulivu kwa nchi za bara zima la Afrika.

Kadhalika Rais Samia amesema utendaji kazi wa baraza hilo katika utatuzi wa migogoro kwa nchi mbalimbali Barani Afrika, inadhihirisha kwamba nchi wanachama zinatambua kuwa baraza hilo lina nafasi muhimu katika kuleta amani na usalama Barani Afrika.

Rais Samia amepongeza mipango ya baraza hilo la amani na usalama katika kusimamia misingi ya haki za binadamu, Demokrasia na utawala bora pamoja kutambua nafasi muhimu ya vijana na wanawake kwenye masuala ya amani na usalama katika ngazi za kitaifa.