Back to top

Hakuna tishio lolote la kigaidi nchini - IGP Sirro.

20 June 2019
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amesema hakuna tishio lolote la kigaidi nchini na kwamba jeshi la polisi lipo imara katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

IGP Sirro amesema hayo jijini Dar es Salaam kufuatia taarifa inayosambaa mitandaoni kuwepo kwa shambulio la kigaidi na kuwatoa hofu wananchi juu ya usalama wao.