Back to top

Hekta elfu mbili katika msitu wa Matogoro Songea zateketea kwa moto

06 November 2019
Share

Hekta elfu mbili katika Hifadhi ya msitu wa mlima Matogoro uliopo wilayani Songea mkoani Ruvuma zimeteketea kwa moto na kuathiri vyanzo vya  maji vilivyoko katika msitu huo.

Afisa  wa wakala wa huduma za  misitu Tanzania (TFS) wilaya ya Songea Juma  Mbwambo anasema kuwa msitu huo umechomwa na watu wanaoandaa mashamba na wachoma mkaa ambao wakati maofisa wa TFS wakihangaika na kuzima moto wao wanapata nafasi ya kubeba mkaa msituni.

Mhandisi wa  mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira manispaa ya Songea (SOUWASA) John Kapinga  anasema kuwa  upatikanaji wa maji  manispaa ya Songea umepungua kutokana na uharibifu wa mazingira kwa kuwa katika msitu huo kuna vyanzo nane vya maji vilivyoathirika kikiwemo chanzo cha mto Ruvuma.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Pololet Kamando Mgema amewataka wananchi  kujiona  sehemu ya misitu na kuilinda na kwamba watakaobainika kuhusika na uhalifu huo watachukuliwa hatua.