Back to top

Iran yakanusha uwezekano wa kutokea vita nchini humo.

19 May 2019
Share

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Bwana.Mohammad Javad Zarif, amekanusha kuwepo kwa uwezekano wa kutokea vita nchini humo, baada ya kupamba moto kwa msuguano kati ya nchi yake na Marekani.

Mwanadiplomasia huyo ameliambia Shirika la Habari la Iran kuwa, nchi yake haitaki kuingia katika mgogoro na hakuna nchi yenye wazo ama inayofikiria kukabiliana nayo katika eneo hilo.

Iran na Marekani zimekuwa katika mvutano baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuongeza vikwazo vya uchumi dhidi ya Iran.

Siku kadhaa zilizopita, uongozi wa Rais Trump uliituhumu Iran kuwatishia wanajeshi wake pamoja na maslahi ya nchi hiyo na kisha Marekani ikapeleka mfumo wa makombora ya kujihami katika eneo hilo.

Iran imeielezea hatua hiyo ya Marekani kuwa ni mchezo wa siasa na vita vya kisaikolojia.