Back to top

JESHI LA ISRAEL KUWAKABILI WANAMGAMBO WA HAMAS

23 July 2024
Share

Jeshi la Israel limetoa amri mpya ya kuwataka Wapalestina waondoke katika sehemu moja ya Ukanda wa Gaza iliyokuwa imetengwa kwa shughuli za kibinadamu.

Mamia ya Wapalestina waliotaharuki wameanza kulikimbia eneo hilo la Al Mawasi lilioko kati ya miji ya Khan Yunis na Rafah.

Jeshi la Israel limetangaza kwamba linapanga kuanza operesheni maalum dhidi ya wanamgambo wa Hamas waliojikusanya kwenye eneo hilo na kulitumia kufyetuwa maroketi kuelekea Israel.

Eneo linalotajwa na Israel linahusisha sehemu ya mashariki ya mji wa Mawasi ambako ni eneo lililotengwa kwa shughuli za msaada, lililoko Kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Tangazo la Israel limekuja katika wakati ambapo maafisa wa Marekani na Israel wameelezea matumaini yao ya kukaribia kufikiwa makubaliano katika mazungumzo tete ya kutafuta usitishaji mapigano.