Back to top

Je,unafahamu faida za bibo la Korosho?

24 May 2019
Share

Kufuatia utafiti uliyofanywa na Taasisi ya utafiti wa kilimo ( TARI) Naliendele Mtwara, umegundua teknolojia mpya ya matumizi ya mabibo ya korosho, kwa kupata aina 3 ya bidhaa inayotokana na mabibo, na kufanya mabibo yawe na thamani kubwa, zaidi ya mara mbili ya korosho yenyewe.

Hayo wamesemwa na mtafiti wa zao la korosho ubanguaji na usindikaji wa matunda katika taasisi hiyo Regina Msoka ambapo anasema baadhi ya bidhaa zinazozalishwa kwa mabibo kuwa ni pamoja na maziwa na jam.

Kwa upande wake mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa tume ya sayansi na teknolojia – COSTECH Dk. Bakari Msangi amepongeza hatua hiyo, lakini akaomba uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mabibo ushirikishe pia taasisi vingine kama Veta na Sido ili kulinda ubora wake.

Bibo la Korosho ya Tanzania ni malighafi ambayo hutumiwa katika maandalizi ya madawa ya kulevya, kuulia wadudu, kutengeneza rangi, plastiki, na kupambana na wadudu walao mbao.

Bibo pia hutumika katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo juice, keki, pipi wiski na aina nyingi za mvinyo kama wanavyofanya kule Brazil.