Back to top

Kiasi kikubwa cha mazao ya mifugo chateketezwa mkoani Arusha.

23 March 2019
Share

Kiasi kikubwa cha mazao ya mifugo yenye thamani ya zaidi milioni 120 zikiwemo kg 8,000 za nyama ya Ngo'mbe iliyokwisha muda wa matumizi imekamatwa ikiwa inaendelea kuuzwa kwenye baadhi ya maduka mkoani Arusha kinyume cha sheria hatua ambayo pia inatishia usalama wa walaji

Akizungumza wakati wa kuteketeza nyama hiyo waziri wa mifugo na uvuvi Mh. Luhaga Mpina pamoja na kuelezea ukubwa wa tatizo la ukiukwaji wa sheria kwenye mazao ya mifugo na uvuvi amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kudhibiti vitendo hivyo huku akiwataka,viongozi na watendaji katika maeneo husika kutekeleza wajibu wao

Akizungumzia operesheni hiyo katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mikoa ya Kilimanjaro,Tanga,Manyara,Kagera, na Mara mwanasheria wa bodi ya nyama nchini na msimamizi wa operesheni hiyo kanda ya kaskazini wamesematatizo la ukiukwaji wa sheria katika mazao ya mifugo ni kubwa na nguvu za ziada zinahitajika.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema serikali inaendelea kuongeza nguvu kuimarisha ulinzi hasa maeneo ya mipakani na vitendo hivyo vitaendelea kudhibitiwa

Katika opreseheni hiyo inayoendelea ikijulikana kama operesheni Zagamba namba 2 Kg.6,395 za nyama na Kg.1,631 za maziwa na Kg.4.95 za vyakula vya mifugo zimekamatwa na wahusika wanaendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na baadhi yao wameshaanza kutumikia adhabu zikiwemo za kutozwa faini .