Back to top

Kunguni wawanyima usingizi  wanafunzi Shinyanga Sekondari.

11 October 2019
Share

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shinyanga wamelalamikia ongezeko la  kunguni katika mabweni na madarasani na hivyo kushindwa kusoma na kukosa usingizi nyakati za usiku.

Wanafunzi hao wametoa malalamiko hayo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi.Zainab Telack alipotembelea shule hiyo baada ya kupata malalamiko ya wanafunzi kupitia wadau wa elimu.

Afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga Mwl.Mohamed Kahundi amekiri kuwepo malalamiko mengi kutoka kwa wanafunzi wa shule hiyo ambayo amekuwa akiyashughulikia kupitia bodi ambapo Mkuu wa Mkoa Bi. Zainab Telack ameagiza changamoto hizo kutatuliwa.