Back to top

IS laua wanajeshi watatu katika mji wa kusini magharibi mwa Libya.

19 May 2019
Share

Maafisa nchini Libya wamesema wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislam (IS) wamewauwa wanajeshi watatu katika shambulizi la kituo cha ukaguzi katika mji wa kusini magharibi mwa Libya.

Taarifa iliyotolewa na jeshi lililojitangazia udhibiti wa eneo la mashariki ya Libya imesema wanamgambo hao pia waliwakamata wanajeshi wanne katika shambulizi hilo kenye mji Zallah lakini watatu kati yao wameokolewa.

Kundi la IS ambalo limethibitisha kuhusika na kisa hicho na mpaka sasa limetanua shuhghuli zake nchini Libya, tangu taifa hilo lillipotumbukia kwenye machafuko baada ya mapigano ya mwaka 2011, yaliyomuondoa madarakani na kuumua kiongozi wa siku nyingi Muammar Ghadafi.

Mji wa Zallah upo kiasi kilimita 750 kusini mashariki ya mji mkuu Tripoli ambapo vikosi vya Jenerali muasi Khalifa Haftar vinapambana kuchukua udhibiti wake kutoka makundi ya wapiganaji yenye mafungamano na serikali dhaifu inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.