Back to top

Lijendari wa Manchester City Glyn Pardoe afariki akiwa na miaka 73.

27 May 2020
Share

Beki wa zamani wa Manchester City Glyn Pardoe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73. 

Pardoe amecheza mechi 380 akiwa na Manchester City tangu mwaka 1962 mpaka 1976 na kufunga bao la ushindi katika ushindi wao wa fainali ya Kombe la ligi 1970 dhidi ya West Bromwich Albion. 

Taarifa hiyo imechapishwa kwenye ukurasa wa Twitter wa klabu hiyo, sambamba na salamu za rambirambi kwenda kwa marafiki na familia yake katika kipindi hiki kigumu.

Pardoe alifanya mazoezi yake ya City mnamo Aprili 1962 akiwa na miaka 15 na siku 341 na alitumia muda wake wote kucheza na klabu hiyo.
  
Mjukuu wake mwenye miaka 18, Tommy Doyle, ambaye ni kiungo, anayecheza katika nafasi hiyo ya kiungo, amecheza mechi yake ya kwanza mwezi Oktoba mwaka Jana, akiwa na Manchester City, mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Southampton na kushinda mabao 3 kwa 1.