Back to top

Mahakama ya Kisutu yapigilia Msumari wa Mwisho kwa Wema Sepetu.

24 June 2019
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imerudishia dhamana yake msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu na kumuonya kwa mara ya mwisho na kumtaka ahakikishe hakiuki tena masharti ya dhamana, vinginevyo haitasita kufutia dhamana yake.

Agizo hilo limetolewa Juni 24, 2019 na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde, wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mshtakiwa huyo kukiuka masharti ya dhamana.

Juni 17, 2019 mahakama hiyo iliamuru mshtakiwa huyo kupelekwa rumande hadi Jun 24, ili iweze kutoa uamuzi baada ya mshtakiwa huyo kujisalimisha mahakamani hapo.

Wema alijisalimisha mahakamani hapo Juni 17, 2019 baada ya Mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kutokana na kushindwa kufika mahakamani bila kutoa taarifa.

Mahakama ya Kisutu, ilitoa hati ya kumkamata Wema, Juni 11, 2019 baada ya mshtakiwa huyo kuruka dhamana.

Wema ambaye ambaye alishawahi kuwa mrembo Tanzania mwaka 2006, anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandaoni wa Istagram kinyume cha sheria.

Hakimu Maira ameaihirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 itakapoanza kusikilizwa.