Back to top

Maombi ya ving'amuzi vilivyofungiwa kuanza kushughulikiwa.

14 May 2019
Share

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Atashasta Nditiye amesema serikali inashughulikia maombi ya makampuni yanayotaka leseni ya kubeba maudhui ya vituo vya televisheni vya ndani ili yaweze kupata leseni stahiki na kuweza kutoa huduma za kubeba na kuonesha maudhui ya ndani kupitia visimbuzi husika.

Naibu Waziri huyo ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyamagana kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Stanslaus Mabula aliyetaka kujua kama serikali  haioni kufungia vingamuzi vya Azam TV, DST na vinginevyo kuonesha vituo vya televisheni vya hapa nchini kuonekana katika vingamuzi hivyo ni kuwanyima haki watu kupata  taarifa.

Mhe.Nditiye amesema serikali inatambua umuhimu wa wananchi kupata fursa ya kujua mambo  yanayoendelea kwenye taifa, kwa misingi hiyo imetoa leseni zenye masharti tofauti ikiwemo leseni za utangazaji wa umma ambapo matangazo huruhusiwa kurushwa na watoa huduma wote.

Amesema kwa sasa matangazo ya umma ni TBC 1 na TBC 3 maarufu kama Safari Channels na kuongeza kuwa makampuni yanayomiliki visimbuzi vya  DSTV, ZUKU na AZAM hayakustahili kutoa huduma ya  kubeba vituo vya televisheni vya hapa nchini kutokana na masharti ya leseni zao.