Back to top

Marekani yatangaza ukomo kuibana zaidi Iran.

28 May 2020
Share


Serikali ya Marekani imeweka ukomo kwenye mpango maalumu ulioziruhusu kampuni za Ulaya, Urusi na China kushiriki katika mradi wa nyuklia wa Iran. 

Kampuni hizo zimepewa muda wa siku 60 tu kuhakikisha kwamba zinakamilisha shughuli zao nchini Iran. 

Utawala wa Rais Donald Trump unafuata sera ya shinikizo kali dhidi ya Iran, kama mkakati wa kuwalazimisha viongozi wa Tehran kukubali mkataba mpya kuhusu mpango wake wa nyuklia ambao utakuwa na masharti magumu zaidi.

Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo aliyeitangaza hatua hiyo ametaka muda kwa kampuni zinazoshirikiana na kinu cha nyuklia cha Bushehr kupewa muda wa hadi siku 90 ziwe zimeondoka.