Back to top

Mashine ya kuchemshia korosho yalipuka na kuua mtu mmoja yajeruhi 2.

12 April 2019
Share

Mtu mmoja amefariki huku wawili wakijeruhiwa baada ya kulipukiwa na mashine ya kuchemshia korosho walipokuwa kwenye mafunzo ya ubanguaji bora wa korosho yanayotolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) mkoa wa Lindi.

Katibu wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine, Bwana.Boniface Lymo amesema leo majira ya saa nne na nusu asubuhi walipokea majeruhi wawili na mtu mmoja akiwa amefariki aliyejulikana kwa jina la Sada Juma mwenye miaka 28 anayetOkoea eneo la msinjaili.

Amesema marehemu alipata majeraha makubwa kwenye eneo la shingo na koo na jeraha hilo limetokana na kukatwa na kitu chenye ncha kali kilichosababisha kuvuja damu nyingi lakini na kupelekea kupoteza maisha .

Tazama video Hapa kuona kila kitu.