Back to top

Meneja bodi ya wadhamini ya watumia maji atafuna milioni 10.

12 July 2019
Share

Naibu Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ameamuru kukamatwa kwa meneja wa bodi ya wadhamini ya watumia maji katika kata ya Heru juu halmashauri ya mji wa Kasulu Kwigize Venance pamoja na wajumbe wa bodi hiyo baada ya kubainika kuiba zaidi ya shilingi milioni kumi na tano za mapato yanayotokana na uuzaji wa maji.

Sambamba na hilo Mhe.Aweso amemuagiza meneja wa wakala wa maji vijijini mkoani Kigoma kuzifuta mamlaka zote za watumia maji ambazo zimeoneka kukiuka sheria ya uendeshaji wa mamlaka hizo.

Amechukua uamuzi huo mara baada ya kupokea malalamiko ya wananchi wa kata hiyo ambao wamedai kushindwa kupata taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi kirefu jambo lililomfanya Naibu Waziri kuchukua maamuzi ya kumkakamata meneja huyo huku akiagiza kutafutwa kwa wajumbe wengine waliosababisha ubadhirifu huo.

Wananchi hao wameishukuru serikali kuchukua uamuzi huo na kueleza kuwa viongozi hao wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwa viongozi mbalimbali wa serikali na kuanzisha migogoro inayosababisha wananchi kuacha kulipia gharama za matumizi ya maji kama sheria inavyoelekeza.