Back to top

Mgodi wa Imalanguzu mkoani Geita wafungwa kwa muda usiojulikana.

09 November 2019
Share

Serikali imetangaza kusitisha zoezi la uokoaji wa wachimbaji wadogo wawili waliofukiwa kwa siku arobaini katika mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Imalanguzu mkoani Geita na kutangaza eneo hilo kugeuzwa kaburi la waliofukiwa.

Akitoa taarifa ya kukwama kwa uokoaji wa wachimbaji hao wawili Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Geita Josephat Maganga amesema serikali imeamua kusitisha zoezi hilo kutokana na mgodi huo kuwa hatarishi kwa waokoaji.

Akitoa kauli ya serikali ya usitishaji uokoaji Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameufunga mgodi huo kwa muda usiojulikana huku familia ,viongozi wa dini walioendesha ibada ya msiba huo wakatoa ujumbe kwa jamii na serkali.

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema migodi mingi ya wachimbaji inahatarisha usalama kutokana na kujengwa kienyeji hasa nyakati hizi za mvua.