Back to top

Mgogoro wa Wafugaji na Wakulima wafukuta kwa miaka 13 Kongwa Dodoma.

18 November 2019
Share

Wafugaji wa Vijiji vya Ngutoto, Chitego na Manyusi Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka zaidi ya 13 kufuatia makundi ya wakulima kutoka Wilaya ya Chamwino kuvamia eneo lilotengwa kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya malisho.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa kujadili namna ya kutatua mgogoro huo, baadhi ya wafugaji wamesema wakulima hao wamekuwa wakivamia maeneo ya malisho na kwamba mgogoro huo umekuwa ukihatarisha hali ya usalama baina ya wakulima na wafugaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Chitego ana ye maliza muda wake, Bw.Harold Wilson amesema mpango bora wa ardhi katika kijiji hicho ulipangwa tangu mwaka 2014, lakini kumejitokeza baadhi ya watu ambao ni wavamizi ambao wameanza kufanya shughuli za kilimo hali inayowafanya wafugaji kukosa maeneo ya malisho.