Back to top

Mkandarasi akamatwa kwa kumdanganya Waziri

18 November 2019
Share

Mkandarasi  wa kampuni inayosambaza umeme wa REA vijini ya  Derm Electrics Mussa Abdallah amekamatwa kwenye  mkutano wa hadhara  katika kijiji cha Mabuyimerafuru mkoani Mara  kwa kosa la kumdanganya waziri  wa nishati Medard Kalemani kuhusu nguzo za umeme za kijiji cha Kichumu zinazodaiwa kukaa zaidi ya miezi mitatu bila kuunganishiwa umeme.

Dkt.Kalemani amechukua uamuzi huo wakati akihutubia wananchi wa kijiji cha Mabuyi merafuru ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua miradi ya umeme na kuwasha umeme ambapo alimwagiza mkuu wa wilaya ya Musoma vijijini,Vicent Naano  kumkamata mkandarasi huyo huku akitoa maagizo kwa mkurugenzi wa wakala wa kusambaza umeme vijijini wa REA kuhakikisha  vijiji vyote vinaunganishiwa umeme kufikia mwishoni mwa mwezi huu na kuwataka   kuweka vituo vya kutoa huduma za malipo kwa wananchi ngazi za vijiji na kata badala ya wananchi kuahangaika kwenda mjini

Aidha akizindua na kukagua miradi hiyo ya umeme Dkt.Kalemani aliwataka wananchi kulinda na kuitunza miundombinu ya umeme huku akiwakabidhi vifaa na kuwasha umeme kwenye nyumba za wananchi  zilizounganishiwa umeme huo wa REA