Taasisi ya mifupa MOI imeanza kufanya upasuaji wa Ubongo bila ya kufungua fuvu la kichwa ambapo upasuaji huo unafanyika kwa kutumia mishipa ya damu pekee ambapo kuazia Januari mwakani huduma hizo zitapanuka zaidi hata kwa wagonjwa kutoka nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Bonifas wakati akizungumza kuhusu Utekelezaji wa shughuli mbalimbali za taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka minne.