Mtaalam na nguli wa lugha ya Kiswahili nchini Makih Hassan ameaga dunia katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam wakati alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya figo.
Marehemu Hassan Makih mbaye amejulikana kwa umahiri wake wa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya lugha ya kiswahili katika kituo cha matangazo ya Radio one.Marehemu Makih amefariki usiku wa tarehe moja majira ya saa mbili usiku.
Wapenzi,wachambuzi na wasomi wabobezi wa lugha ya kiswahili hakika watamkumbuka Hassan Makih kwani ni ndiye miongoni mwa wachambuzi waanzilishi wa kipindi cha Kumepambazuka kiswahili cha Radio one ambacho kinaruka kila Jumamosi.