Back to top

Mtoto wa miaka mitano akutwa na ugonjwa wa ebola Uganda.

12 June 2019
Share

Uganda imethibitisha kuwepo kwa mgonjwa mmoja ambaye ana maambukizi ya homa  ya Ebola wilayani kasese magharibi mwa nchi hiyo.

Wizara ya afya imesema kwamba vipimo kwa mvulana mwenye umri wa miaka 5 vimeonyesha maambukizi ya homa  ya Ebola.

Mtoto huyo anadaiwa kuambukizwa na homa hiyo akiwa  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,wakati familia yake ilipotembelea jamaa katika taifa hilo.

Wizara ya afya imetuma kikosi cha wataalamu wa afya kwenye mipaka na DRC,na kutangaza kuwa itaanza kutoa chanjo Mara moja.

Shirika la afya ulimwenguni (WHO),imetibitisha maambukizi hayo.

Tangu DRC ilipotangaza maambukizi ya homa hiyo mwaka uliopita,Uganda imekuwa katika hali ya tahadhari  kuudhibiti.