Back to top

Muhimbili yatenga vyumba maalum kuwahudumia wajumbe wa SADC.

18 July 2019
Share

Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema imetenga vyumba na wataalam maalum kwa ajili ya kuwahudumia viongozi na wajumbe watakofika katika mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Maendeleo Kusini Mwa Afrika sambamba na kutoa huduma za kitabibu kwa muda wote katika eneo ambalo mkutano huo utakapofanyika.

Akizungumza katika mahojiano maalum na ITV mkuu wa kitengo cha mawasiliano  wa Hospitali hiyo Bwana Aminieli Aligaesha amesema  watahakisha huduma zinapatikana.

Kwa upande wao mamlaka ya masoko na mitaki kupitia mtendaji mkuu wa mamlaka hiyo amesema mkutano huo ni fursa nzuri ya watoa huduma katika sekta ya fedha kuongeza mitaji.

Mhe.Isaya Mwita ni meya wa jiji la Dar Es Salaam ambaye anasema jiji litatumia mkutano huo kama fursa ya kutangaza utalii na nchi kwa ujumla.