Back to top

Museveni kuendelea kuitawala Uganda.

18 April 2019
Share


Mahakama kuu nchini Uganda imeidhinisha mabadiliko ya katiba yaliyoondoa kizingiti cha umri kwa wagombea wa urais nchini humo.

Katika kikao kilichochukua takribani saa 10, majaji wameamua kwamba michakato iliyotumiwa kuifanyia katiba marekebisho haikuhujumu sheria zilizopo.

Katika uamuzi wa majaji 3 kwa 3 wakiongozwa na jaji mkuu Baart Katurebe, mahakama imesema kwamba Bunge ilizingatia ibara ya 79 ya katiba, kuifanyia mabadiliko na kuondoa kizuizi kwa wagombea wa urais.

Ni pigo kubwa kwa upinzani na mashirika ya kiraia yaliyowasilisha kesi hiyo kwa mahakama ya juu nchini humo, 

Sawa na maamuzi ya uongozi wa juu wa chama tawala Cha NRM, ni dhahiri kwamba fursa imefunguliwa kwa Rais Yoweri Museveni mwenye miaka 74 kuendelea kuitawala Uganda hadi atakapopendekeza mrithi wake.

Kabla kipengele Cha katiba kuhusu umri wa wagombea wa urais upitishwe nchini humo,katiba ya nchi hiyo iliwapa Uhuru raia waliochini ya miaka 75 tu kugombea urais.