Back to top

Mwakyembe amwaga sifa kwa Samatta.

18 May 2019
Share

Waziri wa habari ,utamaduni,sanaa na michezo Dk Harrison Mwakyembe amempongeza mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta baada ya kuiwezesha timu yake ya KRC Genk kutwaa ubingwa wa soka wa Ubelgiji.

Mhe.Mwakyembe Amesema Ubelgiji ni moja ya mataifa makubwa yanayong’ara kwa soka duniani na Samatta amefanikiwa kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania.

Samatta, kwa vigezo vyovyote vile, ni shujaa ambaye mchango wake ni mkubwa na tunajaribu kuona ni vipi Samatta anaweza kuwa Balozi wa vivutio vyetu vya utalii, Sanaa na Michezo.