Back to top

Mwili wa kichanga wakutwa katika kizimba cha uchafu Manyoni.

14 October 2019
Share

 

Wananchi wa  Manyoni wa kitongoji cha Majengo wamepatwa na taharuki baada ya kuona mwili wa kitoto kichanga kikiwa kimetupwa kwenye kizimba cha kukusanyia uchafu,huku wakazi wa kitongoji hicho wakilaani ukatili unaofanywa na baadhi ya wanawake wasio kuwa na huruma.


Mwili wa mtoto huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa siku mbili na mzazi wa mtoto huyo bado hajafahamika.
 
Viongozi wa maeneo hayo akiwemo Mwenyekiti wa kitongoji  cha majengo na diwani wa kata  ya Manyoni  wamewaomba wananchi kushirikiana na Jeshi la polisi kusaidia kupatikana kwa mtu aliyehusika kumtupa mtoto huyo.

Akithibitisha kupoke mwili wa mtoto huyo Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Manyoni daktari Furaha Mwakafwila amesema kuwa mtoto huyo anaonekana amekafariki  ndani ya masaa ishirini nanne.