Back to top

Mzee aliyerejesha ekari zaidi ya 200 za ardhi Ukerewe ajinyonga.

10 September 2019
Share

Mkazi wa kijiji cha Gallu katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza Masatu Kezilahabi aliyeamriwa na kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo kurejesha kwenye serikali ya kijiji hicho ekari 193 za ardhi kati ya ekari 200 alizokuwa akimiliki amefariki kwa kujinyonga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Muliro Jumanne Muliro amethibitisha kifo hicho.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe akizungumza na ITV kwa njia ya simu amekiri kupokea taarifa za kujinyonga kwa mzee huyo mwenye umri wa zaidi ya miaka 90.

Septemba 4 mwaka huu, mkuu wa wilaya ya Ukerewe alifika katika kijiji cha Gallu kusuluhisha mgogoro wa ardhi yenye ukubwa wa ekari 200 uliokuwa umedumu kwa zaidi ya miaka 20 bila ufumbuzi na kuamua mzee huyo apewe ekari 7 na ekari nyingine 193 zibaki kuwa mali ya serikali ya kijiji hicho.

Kabla ya kifo chake, marehemu Masatu Kezilahabi aliyekuwa analalamikiwa na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Gallu kumiliki kimabavu ekari zaidi ya 200, alikubali kwa shingo upande kupokea ekari sita alizopewa na kamati ya ulinzi na usalama katika mkutano wa hadhara.
b
Siku hiyo hiyo, wananchi wa kijiji cha Gallu wakiongozwa na mwakilishi wa mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bulemo Celestine walivunja nyumba mbili alizokuwa amejenga marehemu Masatu Kezilahabi, huku mkuu wa wilaya hiyo akitoa utaratibu wa miti na mazao mengine yaliyokuwemo ndani ya shamba hilo.