Back to top

Ndege ya Silverstone Air nchini Kenya, abiria 2 wajeruhiwa.

11 October 2019
Share

Ndege ya kampuni ya Silverstone Air imeanguka katika uwanja wa ndege wa Wilson katika mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Kenya inasema Abiria 50 walikua kwenye ndege hiyo na wahudumu 5, ambapo abiria wawili wamepata majeraha na wanapokea matibabu nchini humo. 

Walioshuhudia wanasema kwamba ndege hiyo ilipoteza mwelekeo wakati ilipokuwa ikipaa kuelekea Mombasa.

Picha kutoka eneo la mkasa zinaonyesha kwamba ndege hiyo ilianguka katika kichaka, ikigonga miti na kuvunja mojawapo ya mbawa zake kabla ya kuangukia ubavu mmoja.