Back to top

Ng'ombe 717 wakamatwa ndani ya msitu wa Pagale wilayani Mvomero.

24 March 2019
Share

Ng'ombe 717 zimekamatwa na kuzuiliwa kwa siku tano mfululizo baada ya kukutwa zikichungwa kwenye msitu wa hifadhi wa Pagale uliopo katika kata ya Mtibwa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro huku wafugaji wanaodaiwa kutenda kosa hilo, kuchunga ndani ya msitu huo wakilalamikia kutakiwa kulipa faini kiasi cha shilingi 15000 kwa kila ng'ombe mmoja.

Wakizungumza na ITV baadhi ya wafugaji hao wamedai kuwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa kila Ng'ombe ni kuwaonea na kutaka kuwafilisi huku wakieleza mifugo hiyo ilikamatwa wakati ikitoka kunywa maji kwenye mto wami.

Kwa upande wake afisa katika hifadhi ya msitu huo wa Pagale Dkt.Hamza Kateti amebainisha uharibifu mkubwa uliofanywa na mifugo hiyo na hatua zilizochukuliwa huku mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero Jonas Vanzeland akianisha sheria za mifugo katika wilaya hiyo inapo chungwa kinyume na taratibu.

Kufuatia kukamatwa kwa mifugo hiyo ITV imemtafuta mkuu wa wilaya ya Mvomero Mwalimu Mohamed Utari ambaye ametoa kalipio kali kwa wafugaji wote wa wilaya ya Mvomero juu ya uharibifu unaofanywa na baadhi ya wafugaji katika misitu ya hifadhi iliyopo katika wilaya hiyo.