Back to top

Nyumba yawaka moto Ruvuma watano wanusurika.

20 April 2019
Share

Watu watano wakazi wa Msamala wilayani Songea mkoani  Ruvuma  wamenusurika kufa baada ya nyumba yao  kuungua moto na sehemu kubwa ya samani za ndani kuungua moto.

Mmiliki wa nyumba iliyoungua moto  bw. Albano Nyandindi anasema moto huo ulitokana na hitilafu ya umeme na ulitokea wakati akiwa  sebuleni na familia yake ya watu watano  na wakati mlipuko wa moto unatokea walikimbia  nje kuita majirani waliosaidia kuzima moto wakati wakisubiri askari wa zimamoto na  watu wa TANESCO waliofika baadaye.

Wananchi waliosaidia kuzima moto wanasema  tukio hilo lilileta taharuki kubwa kwa familia iliyounguliwa na nyumba kutokana na moshi mwingi uliokuwepo ndani ya nyumba hiyo huku pia wakilalamikia tabia ya tanesco mkoa wa ruvuma kukata umeme bila taarifa.

Viongozi wa TANESCO na zimamoto mkoa wa Ruvuma walipotafutwa wazungumzie tukio hilo wameshindwa kupatikana kutokana na kuwa katika mapumziko ya sikukuu ya pasaka huku askari wa zimamoto walioshiriki kuzima moto wakishindwa kuzungumza kwa madai kuwa wao si wasemaji.