Back to top

Nyumba yenye familia Tisa yatekeletea kwa moto Mbeya.

17 September 2019
Share

Familia tisa zimekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi iliyopo mtaa wa Isanga jijini Mbeya kuwaka moto ambao umeteketeza mali zote zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo.

Mmiliki wa nyumba hiyo, Bwana Joseph Michael Mpanji amesema moto huo umesababisha hasara kubwa kwake na wapangaji wake kwa vile vitu vyote vilivyokuwa ndani ya vyumba vya wapangaji wake vimeteketea.