Back to top

Pinda:Kinamama msiwape watoto wachanga asali.

20 May 2019
Share

Waziri mkuu mstaafu Pinda amewatahadharisha wakinamama kuwa makini na matumizi ya asali kwa watoto wachanga,kwa kuwa utumbo wa mtoto unakuwa hauko tayari kuchakata vyakula kama asali.

Ametoa rai hiyo wakati wa maadhimisho ya kwanza siku ya nyuki duniani ambapo amesisiti umuhimu wa ufugaja nyuki ikiwemo mazao yatokanayo na sekta hiyo hususani asali.

Amesema asali imekuwa ikiwapatia kipato baadhi ya wafugaji huku akibainisha kuwepo kwa zana za kisasa za ufugaji wa nyuki ili kuboresha ubora wa asali.