Back to top

Prof.Mbarawa afutilia mbali ongezeko la bei za maji Kondoa na Maswa.

16 September 2019
Share

Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa amefuta ongezeko la bei za maji katika mji wa Kondoa Mkoani Dodoma na Maswa Mkoani Simiyu na kuziagiza mamlaka za maji nchini kudhibiti upotevu wa maji wanayo yasambaza ili kupunguza mzigo wa gharama za maji kwa wananchi.

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo wakati akizindua mradi wa maji unaogharimu Shilingi zaidi ya bilioni 2 katika Kijiji cha Shirima Wilayani Kwimba.

Amesisitiza mamlaka ndogo za maji kuhakikisha zinawafungia wateja wao mita za maji ili kila mtumiaji alipe gharama kulingana na matumizi yake.