Back to top

Rais  Magufuli kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa.

20 November 2019
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli anatarajiwa  kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya Chuo kikuu cha Dodoma kutokana na uongozi wake uliotukuka hususani katika ujenzi wa uchumi wa viwanda kuwekeza kwenye miundombinu pamoja na kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Faustine Bee amesema Mhe rais anakuwa kiongozi wa tatu wa kitaifa kutunukiwa heshima hiyo ambayo hutolewa kwa mtu aliyefanya vizuri katika nyanja mbalimbali akitanguliwa na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dk Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanzania Hayati Rashid Mfaume Kawawa.