Back to top

Rais Magufuli aagiza mapambano ya ujangili wa tembo na faru yaongezeke

09 July 2019
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, amezindua hifadhi mpya ya taifa ya Burigi – Chato, iliyopo katika mikoa ya Geita na Kagera na kuiagiza wizara ya maliasili na utalii kuzidisha mapambano dhidi ya ujangili hasa wa tembo na faru ambao wapo katika hatari ya kutoweka.

Rais Magufuli amefanya uzinduzi wa hifadhi hiyo, ambayo itakuwa ni ya tatu kwa ukubwa, baada ya hifadhi ya taifa ya Ruaha na Serengeti katika kijiji cha Mkolani kata ya Katente wilayani Chato na kuwaonya baadhi ya watumishi wasio waaminifu wa wizara hiyo wanaoshirikiana na majangili kuhujumu maliasili za taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa maliasili na utalii Mh.Dk. Hamis Kigwangalla amewatahadhalisha wanaharakati wa mazingira wa ndani na nje ya nchi ambao wamekuwa wakibeza jiithada za uhifadhi zinazofanywa na serikali kwamba wakiendelea kufanya chokochoko watadhibitiwa.