Back to top

Serikali kuachana na mfumo wa soko huru katika mazao ya kilimo.

15 May 2018
Share

Serikali kupitia Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi ghalani na soko la bidhaa Tanzania inataraji kuanza mfumo mpya wa soko la kilimo na kuachana na mfumo wa soko huru ili kuwahakikishia bei stahiki wakulima kwenye mazao ya ufuta,kahawa na pamba hali itakayosaidia kumpatia mkulima soko la uhakika kwa bei ya haki sokoni.

Akizungumza jijinii Dodoma na wadau wa mazao ya ufuta,kahawa na pamba Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Prof Faustine Kamuzora amesema kupitia mfumo wa soko la bidhaa itawezesha wakulima kuwa na mfumo imara na hatimaye kunufaika na uzalishaji wake kwa kupata bei stahiki sokoni.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa stakabadhi za ghala Agustino Mbulumi amesema wakulima nchini hasa wazalishaji wadogo wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na mifumo imara ya kuuza mazao wanayozalisha.