Back to top

Serikali yagoma kutoa kibali cha uchimbaji kwa mgodi wa GGM

17 November 2019
Share

Serikali imekataa kutoa kibali kwa mgodi mkubwa  wa uchimbaji madini ya dhahabu  wa Geita Gold Minning (GGM) kuendesha uchimbaji wa madini  chini kwa chini kutokana na mgodi huo kushindwa kutekeleza maagizo kumi yaliyotolewa na serikali ikiwemo agizo la  kuwalipa fidia  wananchi zaidi ya mia tatu ambao nyumba zao ziliharibiwa  vibaya na milipuko ya baruti kwa zaidi ya miaka kumi.


Akizungumza mara baada ya kukagua utekelezwaji wa maagizo ya serikali katika mgodi huo waziri wa madini  Mheshimiwa Dotto Biteko ameagiza kuundwa tume maalumu ikihusisha (TAKUKURU) kushughulikia madai ya wanainchi juu ya fidia za nyumba zao ili kumaliza malalamiko ya muda mrefu.


 Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel anasema malalamiko ya fidia kwa wananchi ambao nyumba zao ziliharibiwa na milipuko na zingine kuwekewa vigingi  ni ya muda mrefu na kuundwa kwa tume hiyo kutamaliza kilio cha wananchi

Akizungumzia maagizo ya serikali  kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa GGM makamu wa rais wa mgodi huo Simon Shayo anasema wamepokea maagizo ya serikali na wamejipanga kuziondoa changamoto za fidia kwa wananchi ambao hawajalipwa madai yao.