Back to top

Serikali yajipanga kutoa  matibabu bure kwa wenye seli mundu.

10 June 2019
Share

Serikali inaanza mpango wa taifa wa udhibiti wa magonjwa yasiyoambukiza ambapo ugonjwa wa seli mundu ni moja ya magonjwa yatayokuwa yanaratibiwa kitaifa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe, Dakta Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Taska Mbogo aliyeuliza serikali inampango gani wa kuwasaidia wagonjwa wa seli Mundu kupata matibabu bure.

Dakta Ndugulile amesema serikali kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imeanda mwongozo wa kutoa msamaha kwa makundi tofauti yasiyo na uwezo likiwemo kundi lmeandaa mwongozo wa kutoa msamaha kwa makundi tofauti yasiyo na uwezo likiwemo kundi la watu wenye magonjwa sugu.

Amesema serikali inatambua kuwa wagonjwa wa seli mundu wanahitaji matibabu mfululizo kutokana na kupata maumivu na madhara ya ugonjwa huo mara kwa mara.