Back to top

Serikali yatoa zaidi ya shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya kufanya tafiti

25 May 2018
Share

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia  Profesa Joyce Ndalichako amezitaka Taasisi za utafiti na vyuo vikuu vilivyo pata fedha zaidi ya shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya kufanya tafiti zitakazosaidia kufikiwa kwa malengo ya serikali ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 zinatumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo za mfano wa hundi kwa Taasisi hizo Profesa Ndalichako amesema serikali inadhamira ya dhati ya kuimarisha viwanda na kuendeleza vilivyopo na inategemea tafiti zifanyike ili kuona njia sahihi itakayowezesha kufikia malengo ya uchumi wa kati unaotokana na sekta ya viwanda.

Awali akizungumzia miradi hiyo,Mwnyekiti wa Tume ya Sayansi na Teknolijia Profesa Makenya Maboko amesema uteuzi wa taasisi na vyuo vilivyoshinda tuzo na kupewa fedha hizo umelenga miradi ambayo yenye mchango wa moja kwa moja katika kutekeleza dira ya taifa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo kwa upande wa Tanzania bara zaidi ya shilingi 3 zinatumika katika tafiti na upande wa Zanzabar shilingi Milioni 960 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi minane.