Back to top

Shein atangaza kulegeza masharti ya Covid 19 Zanzibar.

24 May 2020
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj  Dk. Ali Mohamed Shein amesema serikali inakusudia kulegeza masharti ya yaliyowekwa Zanzibar ya kupambana na maradhi ya virusi vya Corona  wakati wowote kuanzia sasa.

Rais Shein ametoa kauli hiyo  katika salamu zake za Eid kwa wananchi wa Zanzibar  baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan  ambapo amesmea hali ya sasa ni nzuri ambapo Zanzibar ina wagonjwa 34 tu.