Back to top

Sheria mpya dawa za kulevya kifungo maisha, Dkt.Shein atia saini.

23 June 2019
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein ametia saini kuidhinisha kuanza sheria mpya ya dawa za kulevya ambapo kuanzia sasa adhabu ya kukutwa na dawa hizo ni kifungo cha maisha jela au faini ya shilingi bilioni moja.

Kutiwa saini kwa sheria hiyo kumetangazwa na Mwanasheria wa Tume ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Zanzibar, Juma Abdulrahman Zidikheri wakti akizumgumnza na wafanyakzi wa Mamlaka ya viwnaja vya ndege katika kutoa taaluma ya sheria na kusema sheria hiyo  imeshaanza kutumika rasmi.

Mwasheria huyo amesemuamuzi huo wa kubadilisha sheria ni endelevu akisema kuanzia sasa adhabu hiyo pia inafaini ya shlingi bilioni moja na ina wakumba hata wale waliotoa msaada.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Vinwaja vya Ndege, Bwana Hamdan Makame amesema sheria hiyo imekuaja wakati muafaka na itaweka heshima ya nchi.