Back to top

Singida yapanga zao la alizeti kuwa moja ya mazao mkakati.

25 May 2018
Share

Serikali  mkoani Singida imepanga zao la alizeti kuwa moja ya mazao mkakati,licha ya kwamba mkoa una mazao  mengine,hii ni kwasababu ya kuweza kutosheleza viwanda vya kukamua mafuta ya alizeti,ikiwemo kiwanda cha Maunt Meru Miller ambacho ni kikubwa Afrika  Mashariki.

Mkuu wa mkoa wa Singida Daktari Rehema Nchimbi amesema hayo wakati alipokuwa akizindua rasmi uvunaji wa zao bora  la alizeti kwenye shamba darasa katika kijiji cha Magida  kata ya Msange Singida vijijini,na kuwataka viongozi   ngazi zote za serikali na dini kuhamashisha ulimaji wa zao hilo.

Kwa upande wake Mkurugunzi mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la faida mali Bwana Tom Silayo anaeleza mchakato wa kupata mbegu bora hapa nchini badala ya kuagiza nje ya nchi kama jinsi ilivyo,huku mkulima Bi.Magreth Issa akieleza ubora wa mbegu hiyo tofauti na ile ya kienyeji. 

Licha ya serikali kuweka mazao mkakati ya pamba,tumbaku,korosho na vitunguu kwa mkoa wa Singida,kuongezewa kwa zao  la alizeti litasaidia kuwanufaisha wakulima kupata soko la uhakika kwasababu mkoa una viwanda vingi vya kukamua  mafuta ya alizeti.