Back to top

Sirro awatahadharisha wakuu wa upepelezi Afrika Mashariki.

16 September 2019
Share

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Tanzania IGP Simon Sirro wamewataka watalaam wa upelelezi na makosa ya jinai katika ukanda wa Afrika Mashariki kuongeza utalaam wa uchunguzi wa  viashiria vya matishio ya ugaidi,uhalifu wa kimtandao,utekaji nyara na dawa za kulevya unaotishia usalama kwenye baadhi ya nchi za Afrika kwa kuwa hakuna nchi iliyo salama.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakurugenzi wa upepelezi wa makosa ya jinai watalaam wa jinai watalam wa masuala ya ugaidi uhalifu wa mitandao na jinsia katika ufunguzi wa kikao wa kamati tendaji ya wakurugenzi wa makosa ya jinai kutoka ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa ni utangulizi wa mkutano mkuu wa wakuu wa polisi katika nchi hizo.

Mkurugenzi wa upelelezi na makosa ya jinai kutoka nchini Kenya Gideon Kimilu anasema kwa hali ilivyo hivi sasa kuna umuhimu wa kuwa na watalaam waliobobea katika masula ya upelelezi kutoka na watenda makosa kubuni mbinu mpya kila kukicha.

Mkuu wa upepelezi na makosa ya jinai nchini Robert boaz anasema hivi sasa wanatarajia kuanza kutekeleza mkakati wa kurekebisha sheria ili zifanane lengo ikiwa ni kuondoa vikwazo vya utekelezaji wa mazimio wanayojiwekea.