Back to top

Spika aliomba Bunge kutoazimia kumsimamisha Mhe.Masele

23 May 2019
Share

Kamati ya Bunge ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge imewasilisha bungeni taarifa ya shauri lililokuwa likimuhusu Mhe.Stephen Masele na kumkuta na hatia na hivyo kupendekeza afungiwe kushiriki mikutano mitatu.

Akiwasilisha taarifa yake mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Emanueli Mwakasaka amesema baada ya kumuhoji Mhe.Masele walimkuta na makosa manne likiwemo la kuchonganisha miimili ya dola, kusafiri nje ya nchi bila ya kibali cha spika na kuandika ujumbe mfupi kwa viongozi wakuu wenye uchonganishi na kudharau wito wa spika.

Hata hivyo Mhe.Masele alipewa ruhusa ya kuomba radhi na kusema anaomba radhi kwa kilichotokea japo alisema katika tuhuma alizotuhuhumiwa yapo mambo mengi ambayo hayapo sawa.

Kwa upande wake Mhe.Spika Job Ndugai adai kuwa Mhe.Masele ni mtu muongo, mfitinishi,mchonganishi na kiongozi ambaye mara nyingi amekuwa akitumia muda wakekugonganisha mihimili na viongozi kwa ujumla.

Kufuatia hatua hiyo Mhe.Spika akaliomba bunge kutoadhimia kumsimamisha Mhe.Masele kama kamati ilivyokuwa imependekeza na badala yake wabunge wampuuze na waachane na suala hilo